Tuesday, 16 February 2016

Ladha ya Penzi (The Taste Of Love) Sehemu ya Tatu.


“Inna my girl! Najua mimi ni msichana na usichana wangu haunizuii kupenda wala kupewa raha wapatazo wanaume” aliongea Solidad kwa kijiamini sana. “Sikia Solidad msichana yeyote aliyakamili kamwe hawezi fanya haya mabo unayotaka kufanya” Inna aliongea akigeukia upande wa pili nakukumbatia mto. “No! usiseme hivyo nahisi mimi ni msichana ambaye sijakamilika kuitwa msichana kwa sababu mbili …….. Moja sina hisia na mwanaume yeyote duniani, pili nina hisia za kimapenzi na wasichana wazuri kama wewe na hata kakazangu wanalitambua hilo na moja kwa moja wanaelewa wewe ni mpenzi wangu but Sorry Inna” aliongea solidad kwa Uchungu uliopitiliza na kumfanya Inna arudishe sura yake upande wake. 

Monday, 15 February 2016

Ladha ya Penzi (The Taste Of Love) Sehemu ya Pili.


   Ni siku ya pekee na nzuri kwa upande wa Inna na familia yake, bila kumsahau Solidad, rafiki kipenzi wa Inna. Ilikuwa ni mahafali ya Inna, Inna alikuwa anahitimu kadato cha nne, Sherehe ilipendeza sana kuanzia shuleni mpaka nyumbani, Baada ya part ya Usiku Solidad aliwaomba wazazi wa Inna aondoke na Inna hadi nyumbani kwao kunazwadi kamuandalia, Wazazi wa Inna hakuweka kipingamizi kutokana na furaha waliyokuwa nayo.

Ladha ya Penzi (The Taste Of Love) Sehemu ya kwanza

     

    Ni usiku uliotulia kwake binti Mrembo Inna, akiwa kitandani akitafakari uzito wa siku inayoelekea ukingoni. Mara ghafla anapatiwa na usingizi.

Inna alishitushwa na sauti ya mama yake iliyosikika ikitokea katika mlango wa chumba chake “wewe mtoto huendi shule, unalala mpaka saa hizi”. Ni sauti na maneno aliyoyasikia Inna na yaliyomfanya akakurupuke toka kitandani, “Naamka mama” Inna alijibu akiwa tayari kishachukua Taulo yake na kwenda kuoga, alijiandaa, akanywa chai tayari kwa safari ya kuelekea shuleni.