“Inna my girl! Najua mimi ni
msichana na usichana wangu haunizuii kupenda wala kupewa raha wapatazo wanaume”
aliongea Solidad kwa kijiamini sana. “Sikia Solidad msichana yeyote aliyakamili
kamwe hawezi fanya haya mabo unayotaka kufanya” Inna aliongea akigeukia upande
wa pili nakukumbatia mto. “No! usiseme hivyo nahisi mimi ni msichana ambaye
sijakamilika kuitwa msichana kwa sababu mbili …….. Moja sina hisia na mwanaume
yeyote duniani, pili nina hisia za kimapenzi na wasichana wazuri kama wewe na
hata kakazangu wanalitambua hilo na moja kwa moja wanaelewa wewe ni mpenzi
wangu but Sorry Inna” aliongea solidad kwa Uchungu uliopitiliza na kumfanya
Inna arudishe sura yake upande wake.
Tendo hilo lilimpa faraja kubwa sana
Solidad. “Solidad stop saying that! What kind of a girl are you?” (Solidad acha
kuongea ivyo wewe ni msichana wa aina gani?) Inna aliongea akionyeshwa
kushangazwa na maneno ya soledad “Nipatie chance Inna nitakuonyesha kwamba
najua kumhendo mschana vilivyo” alisema solidad kwa kujiamini. “But solidad
don’t you know that I have a boy?” (lakini Solidad hujui kuwa nina mwanaume?)
Inna alimuuza Solidad. “Najua lakini sio chanzo cha yeye kunizibia na ninajua
mnapendana sana na Castro, hakuna asiyelijua hilo lakini nipatie chance nami nikuonyeshe mapenzi niliyo nayo kwako”
Castro ni kijana mtanashati
anayefanyakazi kwnye kampuni ya Multichoice Tanzania inayohusika na Usambazaji
wa vifaa vya DSTV pamoja na urushaji wa matangazo kwenye Television. Ni
mwanaume na kijana wa kipekee
aliyempenda sana Inna kwa moyo wake wote na wazazi wao pande zote mbili
walilitambua hilo, “Inna ndiye msichana nitake muoa mimi hakuna mwingine”
Castro alipenda kuyarudia maneno hayo kila anapomkumbuka Inna.
Solidad na Inna walibaki
wakijibizana mpaka ilipohitimu saa nane usiku, Inna aliemdelea kuonyesha
msimamo aliokuwa nao, na Solidad alijitahidi kumbembeleza jinsi awezavyo,
ikafikia kipindi Inna akajuta kumjua solidad na zaidi sana kukanyaga nyumbani
kwao, lakini kwa nguvu ya mapenzi aliyokuwa nayo Solidad aliweza kumshawishi
Inna, nae akajikuta anazama katika penzi la msichana solidad”
Mke wangu mpaka wakati huu uyu
mtoto hajafika bado” mzee Ambachi alikuwa akimuuliza mke wake. “mume wangu na
mimi hata sielewi tatizo ni nini lakini ngoja nipigie simu” aliongea mama
Ambachi akitoa simu yake na tayari kwa kupiga.
Inna
alionekana akiwa kwenye dimbwi la mawazo mara ghafla alishtuliwa na sauti a solidad
akiingia toka Sebuleni “Baby are you owky?”(aliongea Solidad akimfuata Inna
alipokuwa kaketi.
Inna: Ndiyo nipo fresh kabisa
Solidad: Mh! Mbona nakuona uko
out of mood please baby tell me what’s up?
Inna: Hapana solidad nipo sawa
kabisa hata usijali.
Solidad: Do you love me?
Inna: Yap! Nakupenda Solidad,
penzi ulilonipa jana limenifanya nikupende, nisahau hata kurudi nyumbani
mapema.
Solidad: usijali Inna, ntakupa
mapenzi yote, utamsahau hata huyo Castro wako (aliongea Solidad huku akimkumbatia
Inna).
Inna alirudi kwao mchana, kwenye
mida ya saa nane, alisindikizwa na solidad, solidad akiwa kwenye usikani. Baada
ya kufika nyumbani aliagana na Solidad na moja kwa moja aliingia ndani na kupitiliza chumbani kwake, Alishangaa
alipomkuta Castro mpenzi wake akiwa kajilaza kitandani kwake.
“Castro why bila taarifa” Inna
aliuliza kwa mshangao
“kwani nikija kwa mke wangu bila
taarifa kuna kosa” Castro nae aliuliza. “Hapana Castro unajua umenishtua sana”
Castro: usijali Inna, lakini
mbona umechelewa na aliyekushusha na gari hapo nje ni nani?
Inna: Ni rafiki yangu. Anaitwa
Solidad na nilikuwa kwao tangu jana.
Castrro: Mh! Uyo ni msichana au
mvulana nimeangalia vibaya eee! Na mbona amekuaga kwa kukumbatia kimahaba
kabisa.
Inna: (akionyesha ukali) Castro! yule ni rafiki yangu wa kike na hata apa nyumbani wanamfahamu, na kunikumbatia
ivyo ndo unashangaa?
Castro: Sorry Inna mke wangu,
sijamuangalia vizuri “nilijua ni mwanaume(castro akawa mpole tena kwa Inna).
Alimpenda sana lakini upande wa Inna tayari alishachafuka moyoni mwake.
Waliongea mabo mengi lakini Inna alikuwa tofauti na siku nyingine zote na Casto
alilitambua hilo, Alijaribu kumuuliza Inna tatizo nini lakini Inna hakuweza
kumjibu alikuwa tayari kaisha athirika na penzi la Soledad. Inna na soledade
waliendela na mapnzi yao na yaliongezeka siku hadi siku.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Itaendelea Sehemu ya Nne Tafadhili waweza kutoa maoni yako au kushere na marafiki zako
ASANTENI

No comments:
Post a Comment