ILIPO ISHIA:-
Castro: Sorry Inna mke wangu,
sijamuangalia vizuri “nilijua ni mwanaume(castro akawa mpole tena kwa Inna).
Alimpenda sana lakini upande wa Inna tayari alishachafuka moyoni mwake.
Waliongea mabo mengi lakini Inna alikuwa tofauti na siku nyingine zote na Casto
alilitambua hilo, Alijaribu kumuuliza Inna tatizo nini lakini Inna hakuweza
kumjibu alikuwa tayari kaisha athirika na penzi la Soledad. Inna na soledade
waliendela na mapnzi yao na yaliongezeka siku hadi siku.
Ni siku ambayo
hakuitarajia Inna baada ya matokeo yao kutoka, ilikuwa ishapita kama mwaka
mmoja zilitoka post zao ambazo kila mmoja alijitambua anaelekea wapi, Inna hakuamini baada ya kupangiiwa kwenda uingereza kuendelea na masomo yake kutokana na vigezo
vya ufaulu wake kuwa juu zaidi Tanzania nzima. Ilikuwa ni furaha kwake na
familia yake tukimtoa Solidad pekee hakuweza kufurahia jambo hilo akiwa na
sababu zake za kipekee, walipewa muda wa mwezi mmoja wa kuweza kijiandaa, Inna
aliweza kuutumia wakati wote ule kuwa karibu na Solidad wapate kuweza kuagana,
hakuwa na muda na Castro na hata wazazi wake walianza kuligundua hilo lakini
waliamua kukaa kimya na kubaki kusubiri matokeo yanayofuata juu yao.
Castro aliweza kuligundua hilo
lakini aliamua kulifumbia macho na kuwa mpole kabisa kwa Inna akijua alikuwa
anatengeneza kumbe alikuwa akiharibu. Hakuwahi kumuona Solidad akiwa karibu
yake zaidi ya siku ile alipomuona kamshusha Inna kwenye gari hakuweza kumkariri siku
ile na alitamani siku moja amtie Solidad machoni lakini
hakupata nafasi hiyo, alikuwa kapania sana kumona Solidad ili amwambie jinsi
alivyoumia alihisi yeye angeweza kusaidia kwa sababu alikuwa karibu kabisa na
mpenzi wake.
Siku ya kuondoka kwa inna nchini
Tanzania ilitimia, akiwa kwao pamoja na wazazi wake wakijiandaa ili waweze
kumpeleka airport, Alitakiwa kuondoka na ndege ya saa saba mchana na wakati huo
ilikuwa ni saa nne hasubuhi, tayari Inna kaisha wasiliana na kipenzi chake cha
Moyo Solidad Aje amsindikize pamoja na Castro ambaye tayari alikuwa njiani na
alikuja kwa mambo mawili, kumsindikiza mpenzi wake na kumuona solidad na alijua
moja kwa moja siku hiyo angekuwepo maeneo yale ya Airport. Alijiandaa kikamilifu
pamoja na zawadi za mpenzi wake,
Kwa wakati huo Solidad alikuwa akifanya kazi
kwenye kampuni ya Sabedi Transport na masaa yale alikuwa ofisini kwake. Ofisi
yake ilikuwa maeneo ya Sinza. Akiwa mezani kwake simu yake iliita alipoangalia
aliona ni jina la kipenzi chake Inna, Alipokea "hallow baby time zimeenda njoo nyumbani” sauti upande wa pili ilisikia
“ohoo! Sorry baby nakuja sasa hivi ngoja nifunge ofisi” alisema Solidad
akikusanya mafaili yaliyokuwa mezani kwake. Alikata simu na akaanza kusanya faili
zake zote, akatoka na kuanza kufunga ofisi, Mara simu yake tena ikasikika
alkuwa ni kaka yake Declease akimtaka aende nyumbani haraka, na kwa maongezi
yake aligundua kulikuwa na tatizo aliwasha gari haraka hadi nyumbani kwao
alipofika alimkuta declease nje ya nyumba akilia kwa uchungu, alikimbia na kumfua,
alimuuliza nini tatizo declease hakuweza kuongea badala yake alibaki akizidi
kulia. “Haiwezekani!” Ni maneno aliyotamka declease akiwa analia.
Ilichukua
muda kwa decleae kuweza kuongea kilichomfanya awe katika hali ile na Solidad
alijitahidi sana kumbembeleza na kumuomba waingie ndani kwa maongezi mazuri.
Declease alikubali na wakaingia ndani.
Declease aliweza kumweleza dada
yake juu ya taarifa alizozipata kuhusu kifo cha wazazi wao na aliapa kufuatilia
mpaka nchini Canada, Solided aliweza kumweleza kuwa, wazazi wao walishafariki
muda mrefu sasa na alimuomba apotezee na ajikaze kwa taarifa alizopaa lakini
Declease hakuweza kumsikiliza kwa lolote alilosema.
Ni
saa saba kasoro Inna na familia yake pamoja na Castro wakiwa ndani ya gari
wakielekea uwanja wa ndege. Inna hakuwa na raha kabisa kutokana na kutokuwepo
kwa kipenzi chake Solidad, ameshajaribu kupiga simu ni zaidi ya mara kumi lakini
simu haipokelewi, alitamani hata kuhairisha safari yake lakini hakuweza,
alitamani arudishe masaa nyuma aweze kumfuata Solidad lakini haikuwezekana
alibaki akilia tu safari nzima.
Walifika maeneo ya airport bila
mafanikio ya kuonana na soledad, Inna alilia sana alipoangalia saa yake na ndege
ikiwa tayari kwa maandalizi ya safari. Alijikuta anapata hasira alipojaribu
kupiga namba ya solidad bila kupokelewa. “Najaribu mara ya mwisho”
alijisemea Inna huku akilia, alijaribu tena haikupokelewa alijikuta akilia na
kuapata hasira zilizoweza kuonekeana Usoni mwake, Castro alibaki akimwangalia
mpenzi wake kwa huzuni alimwona akiandika SmS na kuzima simu yake kwa hasira aliinuka alipokuwa na kumfuata mama yake na kumkumbatia huku akilia, akatoka na kumfuata baba yake na kumkumbatia akimuaga, Castro aliweza kuyashuhudia hayo Inna
akarudi akamfuata Castro akamkumbatia huku akilia akasogeza kinywa chake karibu na
sikio la Castro akataja herufi ambazo Castro hakuweza kuzielewa “MLWW” ni herufi
alizozitamka Inna kwa Castro na kutoka mikononi mwake kwa kasi na kuiwahi ndege.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Itaendelea Sehemu ya Tano Tafadhili waweza kutoa maoni yako au kushere na marafiki zako
ASANTENI

No comments:
Post a Comment