Monday, 15 February 2016

Ladha ya Penzi (The Taste Of Love) Sehemu ya Pili.


   Ni siku ya pekee na nzuri kwa upande wa Inna na familia yake, bila kumsahau Solidad, rafiki kipenzi wa Inna. Ilikuwa ni mahafali ya Inna, Inna alikuwa anahitimu kadato cha nne, Sherehe ilipendeza sana kuanzia shuleni mpaka nyumbani, Baada ya part ya Usiku Solidad aliwaomba wazazi wa Inna aondoke na Inna hadi nyumbani kwao kunazwadi kamuandalia, Wazazi wa Inna hakuweka kipingamizi kutokana na furaha waliyokuwa nayo.

Majira ya saa mbili Solidad pamoja na rafiki yake mpendwa walitua nyumbani kwao na kuwakuta kaka zake wakiburudika kwa muziki wa polepole, Solidad na Inna waliingia na kuwasalimu Declease na Clease.

      Solidad ni msichana wa pekee katika familia yao, walizaliwa watatu yaani Clease na Declease  ni kaka zake halafu anafuata yeye, Soledad, clease na Declease ni watoto chotara walozaliwa na pande mbili yaani Mtanzania na mhindi ni watoto waliobarikiwa kwa uzuri na akili, Wazazi wao walifariki nchini Canada kwa ajali ya gari na taarifa za kifo cha wazazi wao kila mmoja alizipata kwa wakati wake. Solidad ndio alikuwa wakwanza kupata taarifa hizo na hakuweza kumwambia mtu yeyote, na wapili alikuwa ni Clease nae hakumwambia mtu yeyote na mpaka wakati ule Declease bado alikuwa hajajua taarifa za kifo cha wazazi wao.


      Solidad alibarikiwa kwa uzuri, Sura nzuri na nywele za kishombeshombe alikuwa dizaini kama mwanaume kwa matendo na nyendo zake, hakuwahi kuvaa sketi wala gauni maisha yake, kiufupi Solidad hakuwa na Swagger za kike kwa sababu kampani yake kubwa ilikuwa ni boyz yaani wavulana.

     Baada ya salamu, Solidad alimkaribisha Inna, wakaingia ndani na kuketi, Clease na Declease walionesha mshangao na walijikuta wanazima muziki na kubaki wakimshangaa Inna, kutokana na uzuri aliokuwa nao, Solidad aliwaangalia kakaze na akagundua kitu kutoka kwao “ oya nyie brothers vipi?” alihoji Solidad

 “aha! Sister acha zako ina maana hujui” declease aliitikia. “Sorry, Inna naomba twende ndani tukaongee” Solidad alimuomba Inna, waongozane hadi chumbani, Inna aliingiwa na uwoga uliosababishwa na maneno ya kaka zake Solidad aliinuka na kuanza kumfuata Soledad kwa nyuma wakiwaacha Declease na Clease wakiunguruma na kutoa miguno kwa dada yao kuwaondolea binti mrembo mbele ya macho yao.
 
        Solidad na Inna waliingia chumbani na kuketi kitandani “Sorry Inna wale ni kaka zangu na tunaishi watatu tu humu ndani na hawa wanapenda sana utani So! Naomba uwazoee” alisema Soledad huku mkono wake ukiwa kwenye Bega la Inna. “usiogope Solidad mbona wapo sawa tu” alijibu Inna akiinamisha kichwa chini, waliendelea na story za hapa na pale mpaka ilipotimu saa nne na robo ndipo Inna aliposema anahisi usingizi na kulala akimuacha Soledad akibofya simu yake na laptop ikiwa mbele yake.

       “Nini tena jamani” Sauti ya Inna ilisikika baada ya kushituliwa na mikono iliyomwingilia katikati ya matiti yake, "Samahani Inna, I love you” aljibu Solidad kwa saut ya chini na laini ya kuweza kumtoa nyoka pangoni, Inna alishusha pumzi na kulala tena, “Solidad what the meaning of this” (Solidad nini maana ya yote haya?) Inna alihoji kwa upole “I love you!”(nakupenda) Solidad alijibu kwa mkato, “you are my friend Soledad I know that you love me but think that you are a girl”(wewe ni rafiki yangu Soledad najua unanipenda lakini fikiria wewe ni msichana) alisema Inna kwa hisia kali. 

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Itaendelea Sehemu ya Tatu Tafadhili waweza kutoa maoni yako au kushere na marafiki zako
ASANTENI

No comments:

Post a Comment