Monday, 15 February 2016

Ladha ya Penzi (The Taste Of Love) Sehemu ya kwanza

     

    Ni usiku uliotulia kwake binti Mrembo Inna, akiwa kitandani akitafakari uzito wa siku inayoelekea ukingoni. Mara ghafla anapatiwa na usingizi.

Inna alishitushwa na sauti ya mama yake iliyosikika ikitokea katika mlango wa chumba chake “wewe mtoto huendi shule, unalala mpaka saa hizi”. Ni sauti na maneno aliyoyasikia Inna na yaliyomfanya akakurupuke toka kitandani, “Naamka mama” Inna alijibu akiwa tayari kishachukua Taulo yake na kwenda kuoga, alijiandaa, akanywa chai tayari kwa safari ya kuelekea shuleni.
        Ni kipindi cha break wanafunzi wote walionekana wakiwa nje ya madarasa yao, wengine wakiwa kwenye maduka ya shule, Inna alionekana akitokea darasani akiwa ameambatana na rafiki zake wa kike wawili, ghafla alisikia jina lake likitajwa, aligeuka na kukutanisha macho na binti mrembo, aliyehisi anamzidi uzuri, “Samahani Inna, Jina langu naitwa Solidad” binti Yule alijitambulisha. “eehe Solidad nikusaidie nini?” Inna alihoji, lakini Inna kwa kumuangalia Solidad aligundua kampita darasa kutokana na tofauti ya mavazi  yao. Solidad akiwa form Six na Inna alikuwa form four. 

Solidad: Sorry Inna nilipenda tuwe marafiki, tena marafiki wa karibu sana.
Inna: Unamaanisha nini?
Solidad: Ningependa unijue nikujue tena kwa undani.
Inna: Mh! Poa,(alijibu kwa mkato huku akiguna)
Solidad: So! can I get your number please.?
Inna: Yes you can, (alitoa kikaratasi na kuandika namba zake na kumkukabidhi)
Solidad na Inna waliagana kila mmoja akaendelea na shughuli zake.

Tofauti na alivyotegemea Solidad alijaribu kupiga namba ya Inna ikapokelewa, hakuamini masikio yake kuisikia Sauti ya binti Mrembo Inna, “Hallow” sauti laini ilisikika upande wa pili.
Solidad: yes Hallow!
Inna: Nani Mwenzangu.
Solidad: Solidad naongea, hujambo mrembo?
Inna: am gud! Nambie solidad.
Solidad: Nilihitaji kukusabahi mtoto mzuri, ntakucheki mida
Inna: poa (aliteremsha simu toka sikioni hadi mezani walipokuwa pamoja na mama yake wakipata chakula cha jioni, kisha akaangua, kicheko kilichomfanya mama yake ahoji
“una nini?” mama aliuliza “Hapana mama kuna msichana hapa anahitaji niwe rafiki yakei, mama nashindwa hata kumuelewa” “sasa hicho ndicho kikufanye ucheke”  waliacha kuzungumza na kuendelea kupata chakula

Siku iliyofuata mida ya jioni Inna akiwa anapanga nguo zake alisikia akiitwa na mfanyakazi wao wa ndani akitaarifiwa kuwa kulikuwa na mgeni akimuhitaji nje, Inna alitoka haraka haraka na kumkuta mgeni wake akimsubiri nje, alistaajabu alipokuta ni Solidad, “oho! Solidad Karibu” alimkaribisha ndani na kuketi, alimpatia kinywaji na stori zikaendelea, Solidad hakukaa sana  aliaga na kuondoka, kwa upade wa Inna alibaki na dimbwi la mawazo juu ya vitendo alivyovionyesha Solidad juu yake.

Miezi kadhaa baadae Solidad alikuwa tayari ni mwanafamilia wa mzee Ambachi kulingana na alivyokuwa karibu na Inna na kwa upande wa Inna hakuwahi kufika nyumbani kwao Solidad tangu wajuane, ilikuwa ni kazi ngumu sana kwa Solidad kumbembeleza  Inna hakuwa na wazo la kwenda nyumbani kwa akina Solidad na hakutaka hata kuwajua ndugu zake.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Itaendelea Sehemu ya pili Tafadhili waweza kutoa maoni yako au kushere na marafiki zako
ASANTENI

No comments:

Post a Comment